#mahusiano
Explore tagged Tumblr posts
mwandishiaslam · 8 months ago
Text
Njia za Kumtuliza Mwanaume na Kudumisha Amani na Furaha Ndani ya Mahusiano
Njia za kumroga mwanaume atulie kwenye mahusiano. Ni ndoto ya kila mmoja kuona ndoa yake inakuwa na amani nafuraha huku uaminifu ukiwa ndio mzizi wake. Dhana nyingi huelezea kuwa mwanaumendio huwa msaliti mkubwa linapokuja suala la mahusiano. Lakini dhana kama hiyosi sahihi, kwani usaliti ni hulka ya mtu husika. Lakini pia kwa asilimia kubwa,usaliti huwa unachangiwa na watu wenyewe walio katika…
Tumblr media
View On WordPress
0 notes
lifewithmuhasu · 12 days ago
Text
Jifunze muda sahihi wa kuwaacha waende
Jifunze kuwaacha waende  watu uwapendao ili uweze kupata amani na furaha ya maisha Watu wengi imekuwa mtihani mzito kukubali kuwa wanapaswa kuwaruhusu wawapendao kuondoka kwenye maisha yao wakati mwingine kuwaacha waende ni njia ya kuonesha kuwa unawapenda, unajali na kuheshimu maamuzi yao Watu wengi hujikuta wakikubali uhalisia wa kuwaacha  watu waende baada ya muda mrefu sana kupita bila wao…
1 note · View note
rwizakakiza · 7 days ago
Text
Somo: TABIA 25 ZA KUEPUKA NA HATARISHI KWENYE MAISHA YAKO. (Part 26: WIZ...
youtube
Somo: TABIA 25 ZA KUEPUKA NA HATARISHI KWENYE MAISHA YAKO.
---------------------------------------------------
SUBSCRIBE (Tumaini Jipya Duniani Tv)
Https://youtube.com/@rwizakakiza?si=CC5kjbJiqVUG9vO1
Sehemu: 26.
----------------------
3. 12. TABIA YA 12: "WIZI - THEFT"
Wizi ni tabia ya  kuchukua kitu chochote bila idhini na kwako kuona ni faida. (Mfano..... Kuchukua Habari au kupiga picha, kuchukua pesa, kuchukua mke au Mme wa mtu, au kitu kiwacho chote bila kuomba yaani kupewa idhini na mmiliki yote hayo hutafsiriwa kama wizi).
Shetani uwatia moyo waendelee kuiba maana uona kama faida, wakati wanaiba na kufanikisha hujipongeza na kuendelea na wivi wao, Mfano mtu kuiba mke /mume wa mtu kumwacha ni vigumu, huwa anahisi yupo sawa kumbe ni uongo wa ibilisi, maana ibilisi umwaambia hivi....
.....Maji YALIYOIBIWA ni MATAMU, Na mkate ULIOLIWA kwa SIRI hupendeza.
.....Mithali 9:17.....
Wizi ni hali ya Kudhulumu mtu mali yake, kwa kutumia mabavu au nguvu na kunyang'anya alichonacho bila matakwa yake.
......Msiitumainie dhuluma, Wala msijivune kwa unyang’anyi; Mali izidipo msiiangalie sana moyoni.
..... Zaburi 62:10.....
.....USIMDHULUMU jirani yako, wala KUMNYANG’ANYA mali yake; IJARA yake aliyeajiriwa isikae kwako usiku kucha hata asubuhi.
.......Lawi 19:13......
Wizi ni kitendo cha kuiba . haswa : kuchukua na kuondoa mali ya kibinafsi kwa hatia kwa nia ya kumnyima mmiliki halali yaani kuchukua mali zake kinyume cha sheria za MUNGU au nchi. Wizi ni kuvunja amri za MUNGU na katazo kabisa, ndio maana MUNGU alikataza wizi.
USIIBE.
.....Kutoka 20:15....
MSIIBE, wala msidanganye, wala msiambiane uongo.
.....Lawi 19:11....
Mwizi ni mtu yeyote anayekusudia kuchukua kwa njia isiyo ya uaminifu mali yoyote inayohamishika kutoka kwa miliki ya mtu yeyote bila ridhaa ya mtu huyo , anahamisha mali hiyo ili kuichukua na kuimiliki.
.....Kwa maana HAWAJUI kutenda HAKI, asema BWANA, hao wawekao AKIBA ya JEURI na UNYANG'ANYI katika majumba yao.
......Amosi 3:10.....
Wakati wa kitendo cha wizi kinafanyika na kikafanikiwa uonekana ni faida, Lakini Ukweli ni kwamba unajichimbia kaburi bila kujua. Wizi una madhara makubwa sana, Licha ya kuharibu mahusiano yako na MUNGU na watu pia, Ni chanzo cha mauti yaani kifo.
......Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha, iwapo aona njaa; Lakini AKIPATIKANA, ATALIPA MARA SABA; Atatoa MALI YOTE ya nyumba yake.
.....Mithali 6:30 - 31.....
......Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwivi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
.....Kumb 24:7.....
3. 12. 1. DALILI / MATOKEO YA TABIA YA WIZI.
......Tutaendelea......
________________________________
Rejea
"When Thief is found, he must repay seven times [what he stole]; He must give all the property of his house [if necessary to meet his fine]".
........Proverbs 6:31.......
________________________________
For help:
Ev. Erasmus Pascrates Kakiza
+255 782 546 914
+255 764 215 291
....."2025 KAA NDANI YA YESU, UZAE SANA".....
0 notes
frontlinetv · 2 months ago
Text
Klabu ya Yanga imemtaka Meneja habari na mawasiliano wa Simba SC , Ahmed Ally kutoka hadharani na kuomba radhi kwa matanshi wanayodai yameichafua klabu yao (Yanga) mbali na hili wanadai fidia ya Tsh Bilioni 10
Kauli ya Ahmed iliyosababisha haya 👇
“Pacome amemaliza mkataba tukiona anafaa tutahangaika nae , Pacome amemaliza mkataba ndani ya Yanga na hana mpango wa kuongeza ..mtanyoa ndevu mwaka huu hana mpango wa kuongeza amechoka kuchomwa sindano kila siku kama anazuia mimba”
“Tunaangalia kiwango chake kama kitaturidhisha tutahangaika nae lakini kama ataendelea na mwenendo wake anaoendelea nao tutawaachia…kama tulivyowaachia Chama na tunataja majina Live hakuna kutumia code”
Demand letter ya Yanga imeeleza kuwa kauli hiyo ni ya upotoshaji na imejaa dharau kwa klabu yao , hivyo imeharibu mahusiano yao na wadau wa kibiashara na wadhamini
Yanga wanamtaka Ahmed afanye yafuatayo ndani ya siku tano (5)
1.Kuomba radhi kwa njia sawa na aliyotumia kutoa kauli yake
2.Kufidia malipo ya Tsh Bilioni 10 ( 10,000,000,000)
Yanga wamemaliza kwa kusema kama hayo maagizi hayatafanyiwa kazi watafuata hatua za kisheria zaidi
Kutoka chanzo cha kuaminika.
#frontlinetv
#frontnews
0 notes
mgangakenya · 8 months ago
Link
0 notes
chahali · 8 months ago
Text
0 notes
maxnate-africa · 1 year ago
Text
WhatMax APP NI NINI?
Hii ni aplikesheni ya simu za android itakayokuwezesha wewe mfanyabiashara, muandaa matukio, semina na mikutano kuweza kuwafikia watu wengi ndani ya muda mfupi na kuimarisha mahusiano yenye tija kupitia mtandao wa whatsapp.
INAFANYAJE KAZI?
A: MOJA
Ina uwezo wa kuchukua namba za simu za biashara ama watu waliojisajili katika mitandao ya wazi ya kijamii mfano Google, facebook na kadhalika kwa urahisi kabisa mfano:             Wewe ni mmiliki wa duka la nguo na unauza nguo zako kwa jumla na unahitaji wateja wenye maduka ya nguo wauzao kwa rejareja wa mikoa mbalimbali na nchi mbalimbali ili wanunue nguo kutoka dukani kwako,
utakachotakiwa kufanya katika application ya whatmax ni
i) Hatua ya Kwanza: kuandika aina ya biashara ambayo kwa hapa ni "Duka ya nguo" au "Clothing Store" au "Nguo" na neno lolote linalofanana au kuendana na huduma ya nguo
i) Hatua ya pili: Kuandika eneo la kijografia ambalo unataka kupata namba za simu mfano: kampala, Dodoma, Kisumu nk.
Hatimaye utapata namba zenye mahusiano na ulichoandika na utaweza kuwaweka katika aplikesheni na kuwatumia meseji za whatsapp wote pamoja bila kusevu namba katika simu yako, lakini pia utaweza kuwapigia simu ya kawaida mtu mmoja mmoja kama itakufaa kufanya hivyo..
B: MBILI
WhatMax in uwezo wa kuchukua namba zaidi ya 1000 ndani ya dakika tano tu kutoka katika kundi la whatsapp lolote hata yale makundi ambayo ni kiongozi wa kundi pekee ndiye anaruhusiwa kutuma ujumbe ,
Hivyo kupitia WhatMax utaweza kuwatumia watu wa kwenye kundi meseji, Picha na video kwenye inbox zao bila hata kusevu namba zao
Kumbuka: meseji zinazotumwa kwa mtu binafsi zina uwezekano mkubwa sana wa kusomwa tofauti na meseji zinazotumwa kwenye makundi ya whatsapp.
C: TATU WhatMax ina uwezo wa kuyaweka makundi ya whatsapp unayoweza kuyatumia ujumbe unaofanana yakawa katika kundi moja hivyo utakapotuma meseji moja kutpitia whatMax itaingia kwenye makundi yote yaliyo katika orodha.
Kumbuka: huduma hii ni tofauti kabisa na WHATSAPP COMMUNITY kwani hakuna kundi litalojua kama limeunganishwa pamoja na kundi lingine na meseji au chochote utakachokituma kitakwenda kwenye kundi husika kana kwamba ulituma ujumbe huo kwa kulenga kundi hilo tu. D. NNE WhatMax inakuwezesha kuchukua namba za whatsapp ambazo uliwahi kuchat nazo na hukusevu katika simu yako na kisha kuzitumia meseji.
E. TANO WhatMax ina imewekewa uwezo wa kuwatoa kwenye makundi watu ambao ulikwisha watumia meseji lakini hawakupenda kuendelea kupokea meseji kutoka kwako wakati ujao, na hili linawezekana baada ya kuruhusu mtu aandike  "Unsubscribe" pindi anapopata meseji na kwa namna moja ama nyingine asingependa kupata tena meseji wakati mwingine na hivyo kupunguza kuchukiza watu
F. SITA Kupitia WhatMax utaweza kuwahudumia wateja kulingana na hatua ya uhusiano uliyo nayo inayojulikana kama Customer Journey. Hatua hizo ni kama ifuatavyo;
1. Awareness Katika hatua hii inatakiwa kila mmoja ajue kuhusu bidhaa au huduma yako bila kujali kama atanunua ama hatanunua, na ili huduma yako istawi unatakiwa kuhakikisha kila siku watu wapya wanajua kuhusu biashara yako
2. Consideration Katika hatua hii wale watu ambao walikuwa katika hatua ya kwanza, wakajua biashara yako au huduma unazotoa na wakaonesha kuvutiwa ama kuhamasika na kutamani kujua bei zako, mahali ofisi zilipo, muda wako wa kazi, nk hawa utatakiwa kuwaweka katika kundi tofauti na kuwatumia meseji tofauti na kundi la kwanza
3. Sales
Wale ambao walikuwa katika hatua ya pili lakini wakanunua huduma au bidhaa yako, hawa watatakiwa kutengenezewa kundi lao na watatumia meseji tofauti na kundi la pili
4. Leads Hawa ni wale wateja wa kujirudi hawa watatakiwa kutumiwa meseji za salaamu, heri ya kuvuka mwezi, meseji kuhusu ofa na zawadi kwa kadri ya mpangilio wa huduma yako.
TUMIA WHATMAX APP
Pakua sasa
Tumblr media
1 note · View note
joackcompany · 2 years ago
Text
FAHAMU KUHUSU UFUGAJI WA NJIWA | FAHAMU KUHUSU NJIWA | NJIWA NI BIASHARA
Call/Text/WhatsApp: 0714 63 63 75
@joackcompany @kilimo_tz @mifugo_tz @afyakiganjani @joackagrovet
Muda wetu wa kazi ni saa 1 Asubuhi hadi saa 5 Usiku (7:00am - 11:00pm)
Njiwa ni jamii ya ndege wenye umbo la kiasi, ambao hupatikana duniani kote isipokuwa sehemu zenye baridi kali na kuna zaidi ya aina 250 za njiwa.
Njiwa ni ndege wapole sana, na huwa na mpenzi mmoja tu katika maisha yao, na hawakubali mahusiano mengine mpaka mmoja atapo kufa au kutokuwepo.
Njiwa hutaga mayai mawili tu na kulalia kwa siku 14 hadi 19, Dume hulalia mchana na jike usiku (hulalia kwa kupokezana). Watoto (Makinda) hukaa kwenye kiota kwa siku 12 hadi 18.
Njiwa ndio ndege pekee ambae anazalisha maziwa kwajili ya mtoto wake, maziwa ambaoyo yanaitwa "Pigeon's Milk"
Maziwa ya njiwa (Pigeon's Milk) yanazalishwa na njiwa jike (Stimulated by prolactin hormones) kwenye mfuko wa chakula (Crop), na kuwapa watoto wake walisha totolewa kwa njia ya mdomo.
Kwanini tunafuga njiwa:-
1. Kama pambo
2. Kutumika kwenye michezo
3. Ufugaji wa njiwa ni biashara
4. Ndege wenye upeo mkubwa.
Pamoja na yote, ufugaji wa njiwa huwa na changamoto ya magonjwa japo ni mara chache.
Kuhusu ufugaji wa njiwa, ushauri, matibabu ya njiwa, dawa za kutibu njiwa au kupata njiwa mbalimbali wa urembo, usisite kuwasiliana nasi kwa 0712253102
#njiwa #pigeon #ufugajiwanjiwa #njiwawamapambo #njiwawaurembo #pigeonfarmingi #mayaiyanjiwa#chakulachanjiwa #tunauzanjiwa
Office zetu zipo @Tegetategetawazohill -Barabara ya kwenda kiwanda cha twigacement, opposite na kota za kiwanda - Dar es salaam, Kwa wanaohitaji bidhaa zetu au huduma yoyote fika ofisini au wasilina nasi kwa
Simu:
+255 714 63 63 75(WhatsApp)
+255 692 430 263
Email:
YouTube: https://youtu.be/Yd1kfmho0ac
Website link: https://joackcompany.business.site/
Google location: https://maps.app.goo.gl/C2XiH7ppmYe6pq7Q9
#joackcompany #mifugo #mifugotz #kilimo #kilimotz #sasso #dodoma #tanzania🇹🇿 #morogoro #tanzania #kilimoufugaji #mwanza #dodoma #arusha #mabandayakuku
#tanzaniaweddings
Welcome JOACK Company LTD | DSM & BAGAMOYO
Tumblr media
0 notes
imungy-blog · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Usijiweke kwa mtu, jikite kwenye taasisi. Tumikia taasisi, changia mafanikio ya taasisi, sio mtu. Jenga taswira njema kwa taasisi, usijijengee taswira yako binafsi kama umeajiriwa. Linda maslahi ya taasisi, sio yako binafsi, labda tu kama taswira yako ina tatizo. Linda maslahi ya taasisi, utakuwa umelinda maslahi yako. Usijisemee wewe, semea taasisi yako. Pamoja na malengo yako, kumbuka uko hapo kwa malengo ya taasisi, Ndio maana umepewa hiyo nafasi. Kila kazi Ina mwisho wako. Tabia yako Na matendo yako ndio yatakupa kazi ingine. Kumbuka, watu huajiriwa kwa weledi Na by Eti Vuai ya kuonesha umahiri wa kazi. Wakifukuzwa, hawafukuzwi kwa sababu weledi au vyeti havina tena thamani! Unafukuzwa kutokana na tabia (attitude) zako! Tii viongozi wako, sikiliza ushauri wao. Kiongozi ana mamlaka na sheria pamoja na kanuni za kazi. Zifuate kwa nidhamu, la huwezi, acha kazi hiyo. Ukikisolewa au kuadhibiwa, fuata taratibu. Unyenyekevu Na utulivu ni siri ya mafanikio yako na heshima yako. Hata ukionewa, usipambane, tulia, ukweli siku zote unatabia ya kujidhihirisha. Unaweza usikubaliane Na mimi, inaruhusiwa kukubaliana kutokukubaliana. #carrieradvice #strategicthinking #pr #uhusiano #mahusiano #millardayoupdates #wasafimedia #cloudsdigitalupdates #tbconline @millardayo @cloudsfmtz #mediatraining https://www.instagram.com/p/CRpwhLnss07/?utm_medium=tumblr
0 notes
thenewsbulletnetwork · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Love zone. @modealer_online_tv Wataalamu wa maswala ya mahusiano wanasema kwamba , karne hii tuliyonayo visa na matukio ya watu kuanzisha safari ya mahusiano na ndoa Kisha kuachana ni tatizo jipya la kijamii. "Safari ni hatua" . Safari ya mahusiano ni ndefu hivyo inahitaji sana kujipanga nayo na sio kukurupuka . Ukweli ni kwamba kaa ukijua huwezi kupata mke / mume usieendana nae kitabia na kila kitu huyo uliyempata ndio wako swali kwanini watu huachana? Jibu ni kwamba watu huachana kutokana na matarajio makubwa kutoka kwa wapenzi na waume au wake zao , kaa ukijua huyo iliyenae si malaika kamwe hivyo nae hukosea pia. Lakini ikumbukwe kuwa makosa yaleyale kila siku huwa ni kero sana . Jambo kubwa zaidi linalosababisha mahusiano mengi kuishia njiani ni wenza KUJISAHAU . Kumbuka na simamia majukumu yako katika mahusiano yako . -Weka mawasiliano mazuri kwa mwenza wako -Toa zawadi inapobidi -Pongeza inapobidi -kosoa inapobidi -Epuka matumizi ya nguvu katika kutatua tatizo. -Epuka manyanyaso -Epuka lugha mbaya na chafu. Kumbuka There is no bad girl or boy But There is poor care . #modealer #modealer839#dailymodealer#mahusiano#love#facts#fahamu#wapendanao https://www.instagram.com/p/CQVVNZyj2nb/?utm_medium=tumblr
#love#Tanzania
0 notes
mwandishiaslam · 11 months ago
Text
Shangazi
Tamaa ya kimapenzi, inampelekea Abdam kuwa na mahusiano ya siri na shangazi yake. Tatizo linakuja kuwa kubwa zaidi pale anapoingia ndani ya mtego wa mjomba ake na kujikuta wakikamatwa wakiwa kwenye wimbi zito la mahaba sebuleni. Je unazani nini hatma ya Abdam na familia ya mjomba wake.
Tumblr media
View On WordPress
0 notes
magaratimes · 4 years ago
Text
#VOA. | Biden ajadili mahusiano imara na Canada, Mexico na Uingereza
#VOA. | Biden ajadili mahusiano imara na Canada, Mexico na Uingereza
Hatua ya msukumo huo wa Johnson kufikia makubaliano imekuja wakati wa mazungumzo mapana kati ya viongozi hao yaliyo gusia ulimwengu kukabiliana na janga la virusi vya Corona na tangazo la uongozi wa Biden wiki hii kuwa Marekani itajiunga tena na mkataba wa Hali ya Hewa wa Paris na Shirika la Afya Duniani, kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya Johnson ya Downing Street. Mkataba mpya wa kibiashara kati…
Tumblr media
View On WordPress
0 notes
rwizakakiza · 1 month ago
Text
Somo: TABIA 25 ZA KUEPUKA NA HATARISHI KWENYE MAISHA YAKO. (Part 20: UL...
youtube
Somo: TABIA 25 ZA KUEPUKA NA HATARISHI KWENYE MAISHA YAKO.
---------------------------------------------------
SUBSCRIBE (Tumaini Jipya Duniani Tv)
Https://youtube.com/@rwizakakiza?si=ewqb8Z8S1aeDwoRB
Sehemu: XX.
----------------------
3. 9. TABIA YA 9: "ULEVI - DRUNKENNESS".
Ulevi ni uraibu wa pombe. Ulevi ni tabia au ulemavu unaotokana na UNYWAJI WA POMBE bila KUJIDHIBITI licha ya madhara yake kwa AFYA ya MNYWAJI, MAHUSIANO na HADHI yake machoni pa jamii.
......Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; AKANYWA DIVAI, AKALEWA; akawa UCHI katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, AKAUONA uchi wa Baba yake, AKAWAELEZA ndugu zake wawili waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakaufunika uchi wa baba yao; wala HAWAKUUONA uchi wa Baba yao. Nuhu AKAELEVUKA katika ULEVI wake, AKAJUA mwana wake mdogo alivyomtendea. Akasema, Na ALAANIWE Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
....... Mwa 9:20-25 (SUV) .....
Pombe kwenye maandiko sijaona inapokatazwa kama dhambi, lakini inasababisha Ulevi ambao ni dhambi. Kama ni hivyo pombe haifai na ni katazo kwa sababu pombe inasababisha Ulevi. Hivyo usinywe kabisa maana itajenga tabia ya Ulevi ambapo madhara yake ni makuu mno.
Nuhu alikuwa mkulima, katika ukulima wake akastawisha ZAO linalozalisha pombe, akanywa pombe akalewa mpaka akavua nguo zake akawa uchi. Pombe hiyo ikasababisha alaani uzao wa mwanae. Je kama isingekuwa pombe angekuwa uchi na angewezeza kulaani uzao wa mwanae Hamu?. Je, wangapi kwenye jamii wamepata madhara makubwa kwa sababu ya pombe?.
Je utasemaje pombe ni halali kwa madhara makubwa kiasi hiki?. Najua ninapogusia pombe utakasirika, ila jiulize kwanini unakasirika kama sio mnywaji?. Wengine kuhalalisha pombe yaani Ulevi wanadai... Mbona YESU mwenyewe alitengeneza pombe harusi ya kana?.... Ni kweli Je lengo lilikuwa nini? (Soma mpaka mwisho mstari wa 11).
......Palikuwa na arusi huko Kana, Galilaya; naye mama yake YESU alikuwapo. YESU naye alikuwa AMEALIKWA arusini PAMOJA na WANAFUNZI wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye YESU akamwambia, Hawana divai.......... MWANZO huo wa ishara YESU ALIUFANYA huko Kana ya Galilaya, AKAUDHIHIRISHA UTUKUFU WAKE, nao WANAFUNZI WAKE WAKAMWAMINI.
......Yohana 2:1-11 (SUV)......
Umeona YESU hakutengeneza ila ALIGEUZA na lengo kuu aonyeshe UWEZA wake wa Kimungu ili wanafunzi wamwamini. BWANA YESU anaweza kugeuza chochote kikawa anachokitaka.
Unavyoendelea kuikumbatia pombe na wale wanafanya kufurahisha watu kwa kufanya Sherehe zenye vileo, MUNGU anasema hivi...
.....Wamesababisha watu wengi KUTESEKA. Hivyo hata wao WATATESEKA. Hayo ndiyo malipo yao kwa yale waliyofanya. Wanadhani ULEVI ni jambo la KUFURAHISHA, kutenda dhambi ambapo kila mtu anaweza kuwaona. Wanazifikiria SHEREHE zenye matendo yasiyofaa hata wakati wa mchana kweupe. Hivyo wao ni kama madoa ya uchafu na ni FEDHEHA MNAPOKULA pamoja nao.
......2Petro 2:13 (TKU).....
MUNGU anapokuonya usikubali kutii sauti yake anaruhusu mapepo au Roho ya Ulevi ikutawale wewe na uzao wako ili waangamie kwenye Ulevi wao.
......Ndipo utakapowaambia, BWANA asema hivi, Tazama, NITAWAJAZA ULEVI wenyeji wote wa nchi hii, hata wafalme wanaoketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na makuhani, na manabii, na wenyeji wote wa Yerusalemu. NITAWAGONGANISHA, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; SITAHURUMIA, wala SITAACHILIA, wala SITAREHEMU, hata niwaangamize.
......Yeremia 13:13-14 (SUV).....
Tabia ya Ulevi imesababisha maovu mengi kwenye familia zetu, Mauaji, kutotimiza wajibu, kutelekeza familia, uasherati, matukano, manyanyaso, Ubakaji na kadhalika ingawa wapo watu tena Wakristo wanautetea Ulevi.
Wengine wanatumia pombe kupata haja zao wanazozihitaji kwa kuwalewesha wengine, wengi wamebakwa kwa kuleweshwa, Wengine wamerekodiwa picha za utupu kwa kuleweshwa, Wengine wametenganishwa ndoa zao kwa uzinifu kwa sababu ya kuleweshwa, na wengine wamekuwa wakatili kwa sababu walipoleweshwa walifanyiwa vitendo vya ukatili. Hiyo ni dhambi ya mauti na laana katika uzao wako inayetenda hayo.
.....Mabinti zake WAKAMNYWESHA BABA YAO MVINYO usiku ule, akaondoka huyo mkubwa AKALALA naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, TAZAMA, NIMELALA jana na baba yangu, TUMNYWESHE mvinyo tena usiku huu, ukaingie UKALALE naye. Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
......Mwanzo 19:33-35 (SUV).....
Acha mabaya, acha Ulevi, mkimbilie BWANA YESU Akuokoe.
3. 9. 1. DALILI NA MATOKEO YA TABIA YA ULEVI.
......Tutaendelea......
________________________________
Rejea
"Mwisho wa Ulevi huuma kama nyoka; Huchoma kama fira".
......Mithali 23:32.....
________________________________
For help:
Ev. Erasmus Pascrates Kakiza
+255 782 546 914
+255 764 215 291
@2024 The year of my shining.
0 notes
frontlinetv · 3 months ago
Text
Tumblr media
#frontvibez Kumbe @harmonize_tz hajawahi kuwa na Mahusiano Serious na Binti wa Dini yake (Muislamu).
.
Powered by Joackcompanylimited
.
#frontvibez
#frontlinetv
0 notes
yetusote · 3 years ago
Text
Tumblr media
2 notes · View notes
joackcompany · 2 years ago
Text
FAHAMU KUHUSU UFUGAJI WA NJIWA | FAHAMU KUHUSU NJIWA | NJIWA NI BIASHARA
Call/Text/WhatsApp: 0714 63 63 75
@joackcompany @kilimo_tz @mifugo_tz @afyakiganjani @joackagrovet
Muda wetu wa kazi ni saa 1 Asubuhi hadi saa 5 Usiku (7:00am - 11:00pm)
Njiwa ni jamii ya ndege wenye umbo la kiasi, ambao hupatikana duniani kote isipokuwa sehemu zenye baridi kali na kuna zaidi ya aina 250 za njiwa.
Njiwa ni ndege wapole sana, na huwa na mpenzi mmoja tu katika maisha yao, na hawakubali mahusiano mengine mpaka mmoja atapo kufa au kutokuwepo.
Njiwa hutaga mayai mawili tu na kulalia kwa siku 14 hadi 19, Dume hulalia mchana na jike usiku (hulalia kwa kupokezana). Watoto (Makinda) hukaa kwenye kiota kwa siku 12 hadi 18.
Njiwa ndio ndege pekee ambae anazalisha maziwa kwajili ya mtoto wake, maziwa ambaoyo yanaitwa "Pigeon's Milk"
Maziwa ya njiwa (Pigeon's Milk) yanazalishwa na njiwa jike (Stimulated by prolactin hormones) kwenye mfuko wa chakula (Crop), na kuwapa watoto wake walisha totolewa kwa njia ya mdomo.
Kwanini tunafuga njiwa:-
1. Kama pambo
2. Kutumika kwenye michezo
3. Ufugaji wa njiwa ni biashara
4. Ndege wenye upeo mkubwa.
Pamoja na yote, ufugaji wa njiwa huwa na changamoto ya magonjwa japo ni mara chache.
Kuhusu ufugaji wa njiwa, ushauri, matibabu ya njiwa, dawa za kutibu njiwa au kupata njiwa mbalimbali wa urembo, usisite kuwasiliana nasi kwa 0712253102
#njiwa #pigeon #ufugajiwanjiwa #njiwawamapambo #njiwawaurembo #pigeonfarmingi #mayaiyanjiwa#chakulachanjiwa #tunauzanjiwa
Office zetu zipo @Tegetategetawazohill -Barabara ya kwenda kiwanda cha twigacement, opposite na kota za kiwanda - Dar es salaam, Kwa wanaohitaji bidhaa zetu au huduma yoyote fika ofisini au wasilina nasi kwa
Simu:
+255 714 63 63 75(WhatsApp)
+255 692 430 263
Email:
YouTube: https://youtu.be/Yd1kfmho0ac
Website link: https://joackcompany.business.site/
Google location: https://maps.app.goo.gl/C2XiH7ppmYe6pq7Q9
#joackcompany #mifugo #mifugotz #kilimo #kilimotz #sasso #dodoma #tanzania🇹🇿 #morogoro #tanzania #kilimoufugaji #mwanza #dodoma #arusha #mabandayakuku
#tanzaniaweddings
Welcome JOACK Company LTD | DSM & BAGAMOYO
Tumblr media
0 notes