#wakatiwamunguniwakatisahihi🙏🏽❤️
Explore tagged Tumblr posts
Photo
“Hapo, neno la Mwenyezi-Mungu, lilimjia Elia: “Ondoka uende mjini Sarefathi, karibu na Sidoni, ukae huko. Nimemwamuru mwanamke mmoja mjane akupatie chakula huko.” Basi, Elia akaondoka, akaenda Sarefathi. Alipofika penye lango la mji, alimkuta mwanamke mmoja mjane anaokota kuni. Elia akamwita mwanamke huyo na kumwambia “Niletee maji ninywe.” Yule mwanamke alipokuwa anaondoka, Elia akamwita tena na kumwambia, “Niletee na kipande cha mkate pia.” Huyo mwanamke akamwambia, “Nakuapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wako aliye hai, sina mkate hata kidogo. Nilicho nacho ni konzi ya unga katika chungu na mafuta kidogo katika chupa. Nimefika hapa kuokota kuni, kisha niende nyumbani kupika chakula hicho, mwanangu na mimi tule, kisha tufe.” Elia akamwambia, “Usiogope. Nenda ukafanye kama ulivyosema. Lakini nitengenezee mimi kwanza na kuniletea andazi dogo, kisha jitengenezee wewe na mwanao chakula. Maana, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi: ‘Unga ulioko chunguni mwako hautapungua wala mafuta yaliomo ndani ya chupa hayataisha, mpaka hapo mimi Mwenyezi-Mungu nitakaponyesha mvua nchini.’” Basi, huyo mwanamke mjane akaenda akafanya kama alivyoambiwa na Elia hata mama huyo, jamaa yake na Elia wakapata chakula kwa siku nyingi. Unga chunguni haukupunguka, wala mafuta katika chupa hayakwisha sawa kabisa na neno la Mwenyezi-Mungu alilomwambia Elia aseme.” 1 Wafalme 17:8-16 BHN #ukame:ujumbe wa Mungu watekelezwa-1-7 #Elia na Mama Mjane wa Serefathi;8-16 #Elia amfufua mtoto wa Mama mjane;17-24 #1wafalme17 #wakatiwamunguniwakatisahihi🙏🏽❤️ #stayhome#prayfortheworld #lockdown#covi̇d19 #lifestyleblogger #Rachelsiwa 🙏🏽😔 https://www.instagram.com/p/B-w97JOHVHH/?igshid=15mgoe61f4gsa
#ukame#elia#1wafalme17#wakatiwamunguniwakatisahihi🙏🏽❤️#stayhome#prayfortheworld#lockdown#covi̇d19#lifestyleblogger#rachelsiwa
0 notes