#katy kampa
Explore tagged Tumblr posts
Text
Katy Kampa
151 notes
·
View notes
Photo
HEART EYES 155 Feroz anakua na marafiki wengi kutokana na mishe zake anazofanya, lakini watu wake wa karibu wanakua Lameck na Ibrahim ambao ndo wanakua wakwanza kutambulishwa kwa Maisarah. Kujulikana kwa Feroz kunamfanya Maisarah aanze kuvuma sababu sehemu yoyote ya kujidai anayokuwepo Feroz basi Maisarah hakosekani, kuvuma kwa Maisarah kunazidi baada ya kuonekana kuwa ni mmoja kati ya mabinti warembo zaidi mjini jambo linalomvimbisha Feroz na kumfanya aboreshe maisha ya mpenzi wake kila siku ikiwa ni pamoja na kumlinda baada ya kuona watu wanaweza bila aibu kumpigia misele. Miezi mitano toka wawe wapenzi inabadilisha kabisa maisha ya Maisarah ukiambiwa alikua nati huwezi amini, siku moja Brown anampigia simu Feroz We mzee upo Dar hii? Nipo kaka Inakuaje karibu mwaka unakatika hatuonani kaka? Mishe tuu si unajua mjini Uko wapi wikiend hii maana kuna mtoto kanivuruga naweza kunywa sumu Haha mnywaji sumu anatoa taarifa kaka Ndo hivyo niambie popote nikufate maana namba yako niliipoteza nimepewa muda si mrefu na dogo Pole, niko Masaki nimetulia na wife Hee ushamaliza baba? Siku nyingi Sikuwezi we jamaa, shemeji hana budi kuniona leo Haha poa njoo Sea Cliff Hotel Feroz anakata simu anamkumbusha Maisarah juu ya mtu aliesababisha amuone kwa mara ya kwanza, Maisarah hajawahi kumuona Brown toka arudi normal maana Feroz anawaletea kila kitu hivyo sio yeye wala mama yake wenye sababu yoyote ya kwenda dukani kwa Brown. Brown anafika Sea Cliff Feroz anamueleza walipo, anapokuja Maisarah anakua kampa mgongo moyoni anakiri rafiki yake ni kiboko kwa kuchagua wanawake maana toka shuleni hajawahi muona Feroz na mwanamke asie kifaa Safari hii we jamaa lazima unipe siri nijue hawa watoto wazuri unawaibuaga wapi? Brown anaongea kauli hiyo anapofika pale, wanakumbatiana na Feroz kwa furaha, kabla ya kukaa anampa mkono Maisarah Mambo wife? Poa za wewe? Njema, naitwa Brown ni mume wako namba 2 nimefurahi sana kukufahamu Asante, naitwa Maisarah Kaka hapa nimekubali mtoto anaongea sichoki kumsikiliza daah Acha mambo yako Mzee nimekubali hapa umeoa Haha Shem hongera sana kwa kunitulizia huyu jamaa Maisarah anacheka anamuangalia tuu Brown anaefika na utani mwingi na kushindwa kumtambua..
0 notes