#enockmaregesi
Explore tagged Tumblr posts
best-quotes-top · 6 years ago
Video
youtube
1 note · View note
enockmaregesi · 6 years ago
Photo
Tumblr media
Mwaka huu ungekuwa mwaka wa 88 tangu bibi yangu Martha Maregesi aingie duniani, lakini ni wa 4 tangu aingie kaburini. Kama familia, tunaendelea kuukumbuka ucheshi wake, tunaendelea kuukumbuka upendo wake kwa watu, tunaendelea kuukumbuka upendo wake kwa kanisa, tunaendelea kuzikumbuka sifa zake za ushupavu, tunaendelea kuzikumbuka sifa zake za udhaifu pia. Sala na ibada zinazofanyika makaburini kwa kawaida huwa si kwa ajili ya wale waliokufa, bali ni kwa ajili ya wale waliohai. Hivyo, kwetu sisi tuliohai: Kufa katika Yesu Kristo. Kwani kufa katika Yesu Kristo ni kuishi milele hata milele. Amina. #enockmaregesi #eulogy #grandmother https://www.instagram.com/p/BpvMIfTHTAW/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=s1qrxz3kekb3
1 note · View note
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
DONDOO YA SITA YA KITABU CHA KOLONIA SANTITA KATIKA LUGHA YA KIFARANSA - "La Colonia Santita (CS-14)", poursuivit le Président en se calant dans son siège, " est dans une course pour fabriquer des armes nucléaires selon les services de renseignement de la WODEC, mais nous ne savons pas dans quel but elles sont fabriquées ni avec qui la CS-14 coopère dans ce projet. Nous savons toutefois qu'elle a la capacité et l'expertise nécessaires - et que peut-être elle vendra le plutonium aux gouvernements colombien, iranien ou pakistanais. Selon nos sources au sein de la CS-14, ce minerai et ces stupéfiants sont cachés dans des cotylédons des forêts extraordinaires du Pérou, du Mexique ou de Colombie. La CIA, et d'autre services d'espionnage, qui recherchent le chef de la Colonia Santita depuis plus de dix ans, disent de même que ces cargaisons seront expédiées dans un délai de dix jours à compter d'hier mercredi et qu'elles seront distribuées sur les cinq continents du monde entier", le Président fit une pause et but de l'eau à nouveau. - "Le temps manque", poursuivit le président. "Nous savons à qui appartiennent ces colis. Nous savons qui a tué nos agents de police, les agents des polices mexicaine et américaine, des passants et pour quelle raison il a agi ainsi. Nous ne connaissons pas avec certitude l'endroit où les colis ont été cachés. Arrêter les coupables est une lourde tâche, camarades délégués. Il faut une bravoure exceptionnelle... et se sacrifier. Pour intercepter les colis de la CS-14, et arrêter son chef, il nous faut mener une lutte à mort. Pour que dans dix jours, les cargaisons soient confisquées et détruites et que les chefs (tous) de la Santita soient arrêtés et présentés à la justice". - En savoir plus ici: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=4000247133332418&id=100000415120038 #french #kifaransa #coloniasantita #koloniasantita #enockmaregesi https://www.instagram.com/p/CKygc-vn7A-/?igshid=175trgzohd4ou
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
DONDOO YA NNE YA KITABU CHA KOLONIA SANTITA KATIKA LUGHA YA KIFARANSA Livre: Colonia Santita: La Malédiction du Tigre Auteure: Enock Maregesi, Romancier Africain Couverture: Pas de Couverture de Livre Réelle Le Président de la WODEA est élu par la WGC sur proposition du CSNU. La WBC propose six noms au CSNU qui en retient trois et les présente à la Conférence générale de la WODEA afin de soumettre au vote le poste de Commissaire général de la WODEC et du Président de la WODEA pour une période de cinq ans. Le Commissaire général de la WODEC est le Président de la WODEA. Alors que le WBC se réunit quatre fois par ans à Copenhague à partir de novembre, la WGC (dont 143 pays sont membres) se réunit une fois par an au mois de novembre afin d’approuver le budget et de ratifier les propositions du WBC, ce pour application par le Secrétariat de la Commission mondiale. Le Secrétariat de la Commission mondiale est en charge de l’application de toutes les propositions émises par le WBC et la WGC au nom de la WODEC. Il est élu par le WBC et approuvé par la WGC par périodes reconductibles de cinq ans. Le Secrétariat de la Commission mondiale est aussi responsable d’un effectif de sept mille personnes dans le monde entier et d’un budget moyen de quatre cents dollars américains pour une année complète. En plus du WBC, de la WGC et du Secrétariat général de la Commission mondiale, la WODEC dispose de trois grands appareils régaliens : le Département de Police de la Commission mondiale (WPD), le Département de Sécurité de la Commission mondiale (WIS) et le Groupe Spécial d'Intervention de la Commission mondiale (GSI). Le GSI a été fondé par les accords spéciaux de la résolution de Copenhague entre la WODEA et le Conseil de sécurité de l'ONU en mars 1980. En savoir plus ici: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=3994569090566889&id=100000415120038 #french #koloniasantita #coloniasantita #enockmaregesi https://www.instagram.com/p/CKswuMIHzJq/?igshid=tt543w6t4d7r
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Tarehe 3/6/2020 nilitumiwa baruapepe kutoka kwa rais wa shirika moja kubwa sana huko Swideni akinijulisha kuwa nimependekezwa kuwania tuzo ya kimataifa ya uongozi bora iitwayo Tällberg/Eliasson Global Leadership Prize ya mwaka 2020. Shirika hilo linaitwa Tällberg Organization, na rais huyo anaitwa Alan Stoga. Nilipigwa butwaa, kwa sababu ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kulisikia shirika hilo, na ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kupendekezwa kuwania tuzo kubwa kama hiyo ulimwenguni. Kwa bahati mbaya au nzuri sikushinda tuzo ya mwaka 2020, lakini nilishinda kwa sababu mtu kama mimi niliweza kupendekezwa na shirika kubwa ulimwenguni kutokana na kazi ambayo wengi wanaidharau. Thomas Edson alifeli mara 10,000, kabla ya kugundua taa ya umeme. Mimi ni nani kufeli mara moja tu na nilalamike? - Washindi wa mwaka 2020, miongoni mwa viongozi 2,165 waliopendekezwa ulimwenguni kote, kutoka katika nchi 135, ni hawa wafuatao: Sylvia Earle, mwanasayansi wa bahari; Jared Genser, mwanasheria wa haki za binadamu; na Nithya Ramanathan, injinia na mjasiliamali wa mtandaoni. Kila mmoja aliondoka na kitita cha dola 50,000 za Kimarekani na heshima kubwa duniani ya kushinda Tällberg. Ninawapongeza wote kwa ushindi wenu mkubwa wa kihistoria. Asanteni sana Tällberg Organization, asanteni sana mlionipendekeza, kwa kunipendekeza kuwania tuzo ya Tällberg/Eliasson Global Leadership Prize ya mwaka 2020, kwa sababu ya Nukuu za Nyakati Zetu. Kupendekezwa huko kulinipa faraja na nguvu zaidi ya kutokuwa mwendanguu. Asanteni sana kwa zawadi hii. Maneno yameniishia fikrani. Niwatakie wote kila la heri katika shughuli zenu za kila mwaka za kuwatafuta viongozi bora ulimwenguni. Mungu awabariki sana, ninyi na familia zenu. Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #tällberg #enockmaregesi #sylviaearle #jaredgenser #nithyaramanathan #prizes https://www.instagram.com/p/CKEALNgHhGa/?igshid=87xr2x1hu33c
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Taifa la Muungano wa Visiwa vya Mangrove Vya Ransium, "The United Mangrove Archipelago of Ransium", lililoko katika Bahari ya Pasifiki, mwaka jana lilininukuu katika mojawapo ya mikutano yake ya kimataifa inayohusu mazingira. Taifa hili, kwa mtazamo wangu, ni taifa lenye mambo ya kushangaza sana! Kwa mfano, hakuna Serikali Kuu. Linaendeshwa na serikali za mitaa, na linaamini katika dini iitwayo "Mangrovism" ambayo ni dini ya misitu. Aidha, katika Jamhuri ya Ransium kuoa wake au waume wengi kumeruhusiwa kikatiba kabisa! Ndoa za jinsia moja zimeruhusiwa pia. Pia mtu anapokufa viungo vyake vyote muhimu lazima vitolewe kwa ajili ya kafara, au kwa ajili ya walio hai wanaovihitaji kwa ajili ya afya zao. Katika taifa hilo watoto hujitunza wenyewe. Yaani, hawatakiwi kupata matunzo kutoka kwa wazazi wao au jamii yao ya Kiransium na wanaruhusiwa hata kufanya kazi za kujikimu kwa ajili ya maisha yao wenyewe. Hakuna michezo ya aina yoyote ile wala hakuna kuvuta sigara au mihadarati, na kafara za binadamu zinaruhusiwa bila kificho kwa sababu za kidini. Katika taifa la Ransium hakuna kompyuta, hakuna intaneti, hakuna magari, hakuna ndege (eropleni), na hakuna pombe ya aina yoyote ile. Nilijisikia furaha sana kunukuliwa na taifa linaloongoza kwa utunzaji wa mazingira duniani, ambalo Umoja wa Mataifa ulilichagua kuwa balozi wake wa misitu toka Machi 20 mwaka 2007. Hili ni taifa ambalo watu wengi duniani hawalijui. Haliko kwenye ramani ya Dunia. Liko katikati ya Bahari ya Pasifiki, likiwa na jumla ya visiwa vikubwa 16 vinavyojitegemea; na kwa mujibu wa NSWIK, http://archive.nswiki.org/index.php?title=Ransium, unaambiwa lina watu zaidi ya bilioni 1.4, zaidi ya China au India au Afrika! - Halafu taifa hilo linahamasishwa na nukuu ya Mtanzania ambaye hata hakuujua uwepo wake! Asante sana Ransium kwa kuninukuu, na kwa kuifanya nukuu yangu kuwa kaulimbiu ya mkutano wenu wa majuma mawili kuhusu misitu ya mikoko mnayoithamini sana. Mungu ibariki Ransium. Mungu wabariki Waransium. Soma zaidi hapa: https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=3948955368461595&id=100000415120038 #ransiumarchipelago #nationstates #wastates #enockmaregesi #mangroveforest #environment https://www.instagram.com/p/CKDSreeHZIs/?igshid=daftixh6qqua
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Tarehe 2 Oktoba 2020 Debbie Dingell (D-MI), Mbunge wa Bunge la Congress la Marekani, alininukuu katika moja ya machapisho yake huko Washington D.C. akionesha hisia zake chanya dhidi ya Rais Donald Trump baada ya Trump kuugua ugonjwa mbaya wa UVIKO-19. Debbie Dingell alichukua kijiti cha ubunge wa Michigan toka kwa mumewe John Dingell mnamo mwaka 2015, baada ya Mzee Dingell kulitumikia Bunge la Marekani kwa tiketi ya Chama cha Democratic tangu mwaka 1955; huku yeye pia akichukua kijiti cha ubunge huo kutoka kwa baba yake, aliyejulikana pia kama John Dingell, aliyekuwa mbunge wa Michigan kuanzia mwaka 1933—1955 alipofariki dunia. Ahsante sana Debbie Dingell kwa kuichagua nukuu hii kuwa nukuu bora ya siku miongoni mwa misemo mingi unayoijua, na hasa kwa kunitambua katika blogu yako wewe kiongozi mkubwa namna hiyo na unaeheshimika sana. Nakutakia kila la heri katika shughuli zako zote. Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #debbiedingell #enockmaregesi #benice https://www.instagram.com/p/CKB2uNZnuoA/?igshid=1ug9xp266tib2
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Katika jarida la kiroho liitwalo 'Because' la huko Uingereza nilinukuliwa na James Henderson, mwandishi wa jarida hilo, anayesimulia jinsi alivyoipoteza dini yake huko Uskochi, katika ukurasa wa 7, kuhusiana na umuhimu wa maneno katika ujenzi wa maisha na dunia yetu. Asanteni sana 'Because' na James Henderson, kwa kunitambua katika jarida lenu hili zuri sana la mwaka 2019! Hakika maneno tunayoyafikiria na kuyaongea yana nguvu kubwa sana ya kuibadilisha dunia yetu. Mungu awabariki sana. Lipate jarida hili kwa kunitumia anuani yako ya baruapepe hapa. Au tembelea tovuti ya jarida hilo: www.because.uk.com kupata taarifa zake. Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #because #jameshenderson #enockmaregesi #wordsofwisdom #words https://www.instagram.com/p/CKBKB9OHrb6/?igshid=12gbw1plgskvv
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Asanteni sana Chuo Kikuu cha Cornell, New York, kwa kutukumbuka kupitia jarida lenu la Africana toleo la mwaka 2015. Asante sana. #africana #cornelluniversity #enockmaregesi #annasamwel #mabaticornellawards https://www.instagram.com/p/CJ-wNcLHl1b/?igshid=13xqnn17k1nls
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Jifunze jambo kutoka kwa waandishi bingwa wa riwaya; hapo tukiwa katika studio za KBC, Nairobi, Kenya, mwishoni mwa mwaka 2015. #kbc #enockmaregesi #annasamwel #nairobi #kenya🇰🇪 https://www.instagram.com/p/CJ-qzawnFVY/?igshid=lhpak08r2dys
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Katika jarida la ndege liitwalo "Quail" la Eugene, Oregan, Marekani, la Oktoba mwaka 2016, nilinukuliwa na Debbie Schlenoff—mwandishi wa jarida hilo—kupitia mojawapo ya nukuu za "Nukuu za Nyakati Zetu", kitabu changu cha KIROHO. Kupitia nukuu hiyohiyo na kupitia mwaka huohuo nilinukuliwa kabla na Anne Kidmose Jensen wa gazeti la "Citizen" la Afrika Mashariki, kutokana na mahojiano maalumu niliyofanya naye sehemu fulani katika jiji la Dar. Asante sana Audubon Society of Lane County, wamiliki wa jarida hilo, Debbie Schlenoff, na Anne Kidmose Jensen kwa kunitambua katika jarida na gazeti lenu. Ni imani yangu kuwa kipo kitu hadhira yenu ilijifunza kutokana na ujumbe huo. Asanteni sana, na Mungu awabariki sana. Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #thequail #words #enockmaregesi #eugen #thecitizen #debbieschlenoff #annekidmosejensen https://www.instagram.com/p/CJ-mKcBHbyv/?igshid=1o8850p71j0m1
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Katika jarida la wanyama liitwalo "Voice for Animals" la York, Maine, nchini Marekani, katika toleo lake la Aprili la mwaka 2015, nilitajwa katika ukurasa wa 5 pamoja na paka wawili wazuri wajulikanao kama Jasmine na Niles (ajulikanaye pia kama Niles Wadsworth Longfellow). Hapo tulinukuliwa waandishi wanne: Karen Davidson, Elizabeth Parker, Charles Dickens, na mimi Enock Maregesi. Asanteni sana "Voice for Animals" kwa zawadi, ya kunitambua katika jarida lenu hili la mwaka 2015! Mimi pia ni mpenzi sana wa wanyama. Ndiyo maana mwaka 2009 niliitunga nukuu hii, kwa minajili ya kuwatetea wanyama wote kote ulimwenguni. Nukuu hii imehamasishwa zaidi na mashirika mengi yanayowatetea wanyama ulimwenguni kote. Huwa inanipa faraja sana ninapoona watu kama nyie mkiitumia, tena kwa usahihi! Nawatakia wote heri na fanaka katika shughuli zenu zote za kuwatetea wanyama. Enock Maregesi, mwandishi wa Kolonia Santita #voiceforanimals #enockmaregesi #karendavidson #elizabethparker #charlesdickens #animal #animalsofinstagram #animals https://www.instagram.com/p/CJ8y4MaJleR/?igshid=1l1hhzab08rzm
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Katika kitabu cha "Naturalopy: The Complete Reference" tumetajwa Waafrika watano tu: Chimamanda Ngozi Adichie, ukurasa wa 73 Nelson Mandela, ukurasa wa 245, 312, 572, 874, na 890 Kalu Igwe, ukurasa wa 573 Enock Maregesi, ukurasa wa 848 Desmond Tutu, ukurasa wa 997 Nukuu ya Kiyoruba, ukurasa wa 456. Kitafute kitabu hiki bora kabisa ili ujue ni nini kilichomhamasisha Mwandishi Trung Nguyen hata kutuandika sisi sita katika kitabu chake, kinachozungumzia ubinadamu kwa ujumla wake na chenye maarifa makubwa. Tembelea tovuti ya Nguyen hapa: www.encognitive.com Asante sana Trung Nguyen, mwandishi wa "Naturalopy: The Complete Reference", kutoka Edmonton, Alberta, Kanada, kwa kututambua katika kitabu chako kuntu. Kitabu hiki ni kwa ajili ya watu waliopevuka kiakili. Kina kurasa 1113! Binafsi nimekisoma chote mara mbili. #trungnguyen #naturalopy #chimamandaadichie #nelsonmandela #kaluigwe #enockmaregesi #desmondtutu https://www.instagram.com/p/CJyXAnwHmjq/?igshid=r36v3nyzwwdt
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Nukuu hii imetumika zaidi kama kaulimbiu ya kliniki nyingi za madawa ya kulevya na pombe ulimwenguni. Hapa imetumika katika Kliniki ya Galino Recovery Centre ya nchini Afrika Kusini. Asanteni sana Galino House kwa kunitambua, nawatakia kila la heri katika mahangaiko yenu. #galinohouse #rehab #addictionrecovery #enockmaregesi https://www.instagram.com/p/CJyVfUPHvKN/?igshid=1d095dnsd5aw5
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
Asanteni sana Una Tanzania, Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania, kwa nukuu hii kumhusu Mwalimu. Mwalimu Nyerere alikuwa baba kwa familia yake; lakini kwa Tanzania, alikuwa mlezi wa ndoto. Anaishi, kiroho, kupitia kumbukumbu za wengi aliotuacha duniani, na ataishi hivyo kwa muda mrefu sana. Nawatakia kila la heri. #unatanzania #juliusnyerere #enockmaregesi #tanzania🇹🇿 https://www.instagram.com/p/CJyUVpRHe77/?igshid=1ss77nuxevn8p
0 notes
enockmaregesi · 4 years ago
Photo
Tumblr media
We are the children of Nelson Mandela; we are the children of Kwame Nkrumah; we are the children of Haile Selassie; we are the children of Samora Machel; we are the children of ­Robert Mugabe; we are the children of Patrice Lumumba; we are the children of Julius Kambarage Nyerere. We know who we are. #nelsonmandela #kwamenkrumah #haileselassie #samoramachel #robertmugabe #patricelumumba #juliuskambaragenyerere #enockmaregesi https://www.instagram.com/p/CDGH8z-HdEJ/?igshid=hi8b6146j63n
0 notes