#akapanda
Explore tagged Tumblr posts
Text
Somo: TABIA 25 ZA KUEPUKA NA HATARISHI KWENYE MAISHA YAKO. (Part 20: UL...
youtube
Somo: TABIA 25 ZA KUEPUKA NA HATARISHI KWENYE MAISHA YAKO.
---------------------------------------------------
SUBSCRIBE (Tumaini Jipya Duniani Tv)
Https://youtube.com/@rwizakakiza?si=ewqb8Z8S1aeDwoRB
Sehemu: XX.
----------------------
3. 9. TABIA YA 9: "ULEVI - DRUNKENNESS".
Ulevi ni uraibu wa pombe. Ulevi ni tabia au ulemavu unaotokana na UNYWAJI WA POMBE bila KUJIDHIBITI licha ya madhara yake kwa AFYA ya MNYWAJI, MAHUSIANO na HADHI yake machoni pa jamii.
......Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; AKANYWA DIVAI, AKALEWA; akawa UCHI katika hema yake. Hamu, baba wa Kanaani, AKAUONA uchi wa Baba yake, AKAWAELEZA ndugu zake wawili waliokuwa nje. Shemu na Yafethi wakaufunika uchi wa baba yao; wala HAWAKUUONA uchi wa Baba yao. Nuhu AKAELEVUKA katika ULEVI wake, AKAJUA mwana wake mdogo alivyomtendea. Akasema, Na ALAANIWE Kanaani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
....... Mwa 9:20-25 (SUV) .....
Pombe kwenye maandiko sijaona inapokatazwa kama dhambi, lakini inasababisha Ulevi ambao ni dhambi. Kama ni hivyo pombe haifai na ni katazo kwa sababu pombe inasababisha Ulevi. Hivyo usinywe kabisa maana itajenga tabia ya Ulevi ambapo madhara yake ni makuu mno.
Nuhu alikuwa mkulima, katika ukulima wake akastawisha ZAO linalozalisha pombe, akanywa pombe akalewa mpaka akavua nguo zake akawa uchi. Pombe hiyo ikasababisha alaani uzao wa mwanae. Je kama isingekuwa pombe angekuwa uchi na angewezeza kulaani uzao wa mwanae Hamu?. Je, wangapi kwenye jamii wamepata madhara makubwa kwa sababu ya pombe?.
Je utasemaje pombe ni halali kwa madhara makubwa kiasi hiki?. Najua ninapogusia pombe utakasirika, ila jiulize kwanini unakasirika kama sio mnywaji?. Wengine kuhalalisha pombe yaani Ulevi wanadai... Mbona YESU mwenyewe alitengeneza pombe harusi ya kana?.... Ni kweli Je lengo lilikuwa nini? (Soma mpaka mwisho mstari wa 11).
......Palikuwa na arusi huko Kana, Galilaya; naye mama yake YESU alikuwapo. YESU naye alikuwa AMEALIKWA arusini PAMOJA na WANAFUNZI wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye YESU akamwambia, Hawana divai.......... MWANZO huo wa ishara YESU ALIUFANYA huko Kana ya Galilaya, AKAUDHIHIRISHA UTUKUFU WAKE, nao WANAFUNZI WAKE WAKAMWAMINI.
......Yohana 2:1-11 (SUV)......
Umeona YESU hakutengeneza ila ALIGEUZA na lengo kuu aonyeshe UWEZA wake wa Kimungu ili wanafunzi wamwamini. BWANA YESU anaweza kugeuza chochote kikawa anachokitaka.
Unavyoendelea kuikumbatia pombe na wale wanafanya kufurahisha watu kwa kufanya Sherehe zenye vileo, MUNGU anasema hivi...
.....Wamesababisha watu wengi KUTESEKA. Hivyo hata wao WATATESEKA. Hayo ndiyo malipo yao kwa yale waliyofanya. Wanadhani ULEVI ni jambo la KUFURAHISHA, kutenda dhambi ambapo kila mtu anaweza kuwaona. Wanazifikiria SHEREHE zenye matendo yasiyofaa hata wakati wa mchana kweupe. Hivyo wao ni kama madoa ya uchafu na ni FEDHEHA MNAPOKULA pamoja nao.
......2Petro 2:13 (TKU).....
MUNGU anapokuonya usikubali kutii sauti yake anaruhusu mapepo au Roho ya Ulevi ikutawale wewe na uzao wako ili waangamie kwenye Ulevi wao.
......Ndipo utakapowaambia, BWANA asema hivi, Tazama, NITAWAJAZA ULEVI wenyeji wote wa nchi hii, hata wafalme wanaoketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na makuhani, na manabii, na wenyeji wote wa Yerusalemu. NITAWAGONGANISHA, mtu na mwenzake, naam, baba za watu na watoto wao pamoja, asema BWANA; SITAHURUMIA, wala SITAACHILIA, wala SITAREHEMU, hata niwaangamize.
......Yeremia 13:13-14 (SUV).....
Tabia ya Ulevi imesababisha maovu mengi kwenye familia zetu, Mauaji, kutotimiza wajibu, kutelekeza familia, uasherati, matukano, manyanyaso, Ubakaji na kadhalika ingawa wapo watu tena Wakristo wanautetea Ulevi.
Wengine wanatumia pombe kupata haja zao wanazozihitaji kwa kuwalewesha wengine, wengi wamebakwa kwa kuleweshwa, Wengine wamerekodiwa picha za utupu kwa kuleweshwa, Wengine wametenganishwa ndoa zao kwa uzinifu kwa sababu ya kuleweshwa, na wengine wamekuwa wakatili kwa sababu walipoleweshwa walifanyiwa vitendo vya ukatili. Hiyo ni dhambi ya mauti na laana katika uzao wako inayetenda hayo.
.....Mabinti zake WAKAMNYWESHA BABA YAO MVINYO usiku ule, akaondoka huyo mkubwa AKALALA naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, TAZAMA, NIMELALA jana na baba yangu, TUMNYWESHE mvinyo tena usiku huu, ukaingie UKALALE naye. Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
......Mwanzo 19:33-35 (SUV).....
Acha mabaya, acha Ulevi, mkimbilie BWANA YESU Akuokoe.
3. 9. 1. DALILI NA MATOKEO YA TABIA YA ULEVI.
......Tutaendelea......
________________________________
Rejea
"Mwisho wa Ulevi huuma kama nyoka; Huchoma kama fira".
......Mithali 23:32.....
________________________________
For help:
Ev. Erasmus Pascrates Kakiza
+255 782 546 914
+255 764 215 291
@2024 The year of my shining.
0 notes
Text
Usimkimbie Mungu
Basi neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu. Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa…
View On WordPress
0 notes
Photo
Usimcheke wala kumdharau abiria aliyesimama tangu mwanzo wa safari. Wakati wake wa kupata kiti bado, lakini yumo safarini! Hivi majuzi nilisoma post moja humu instagram inayofanana na ujumbe mzito alioniusia Marehemu Mama yangu Mangowi (R.I.P Maa) kuhusu maisha. Posti hiyo ilinigusa (sikumbuki nani aliposti) na kunikumbusha maneno ya Mangowi kuhusu maisha, kazini na hata kwenye shughuli za kijamii au biashara, hata siasa pia. Alilinganisha shughuli hizo Na safari ya basi. “Maisha ni kama kuwa kwenye safari ya basi lililojaa tangu umeanza safari (ajira, biashara, siasa, utumishi katika dini nk). Usimcheke aliyekosa kiti Na akashika bomba tangu mwanzo hadi mwisho kwa vile umekaa kwenye kiti, kila mtu ana bahati yake, wakati wake na muda wake maalumu kupata kiti akae”, alisema Msheku. Majuzi nilifikiria sana huu ujumbe Baada ya kuulizwa swali Na wenzangu kuwa lini na wao watatambulika na kuonekana kama wengine? Niliwajibu kuwa kila mtu amepangiwa maisha yake na inahitaji subra wakati wako ufike. Nilitoa mfano wa wasafiri kwenye basi la mwendokasi kutoka mbezi mwisho hadi kivukoni. Niliwaambia Usimuonee wivu aliyepandia Mwembechai na kupata kiti hapo hapo baada ya mwingine kushuka. Endelea kushika Bomba, Bado uko safarini, muda wako wa kupata kiti bado. Aliyepandia Mwembechai, anaweza kushuka Magomeni na mwingine akapanda na kupata kiti. Usipate wivu, endelea kushika bomba bado muda wako. Hata ikitokea ukafika mwisho wa bus Kivukoni bila kupata kiti, isikusumbue, shuka na endelea na mambo yako. Ndivyo maisha yalivyo. Kutokupata kiti hakuzuii wewe kufika mwisho wa safari. Na waliokaa kwenye viti sio muhimu kuliko wewe, ni wakati wao, ikuwa wakati wako Na wewe utapata kiti. Ridhika na nafasi yako katika maisha, kazini, kwenye huduma, biashara na hata darasani. Endelea kushika bomba, muda wako wa kupata kiti utafika, usipopata kiti usiumie, shika bomba umalize safari yako. Ungejua wanayopitia waliokaa, unaweza usitamani kukaa. Viti vingine vibovu vinaumiza, wengine watashuka kabla yako, wengine watashushwa kwa simu za dharura nk. Songa mbele na safari yako. Hata ukikanyagwa wakati umesimama, vumilia, kila safari ina mwisho. Wote tuko safarini. https://www.instagram.com/p/CPe4FDwsWBI/?utm_medium=tumblr
1 note
·
View note
Text
3. KUKOSA UTIIFU KATIBU BUSTANI YA EDENI
“Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni”
Shabaha
Ni kuonyesha nini kilitokea baada ya Adamu na Hawa kutomtii Mungu.
Muhtasari
Mungu alikuwa ametayarisha bustani nzuri kwa ajili ya kuishi mwanaume na mwanamke ili waishi ndani yake. Iliitwa busani ya Edeni. Likiwa na maana ya “furahia”. Ilikuwa na miti mingi ya kupendeza kwa kuiangalia na pia mizuri kwa chakula. Mto ukiimwagilia bustani na Adamu aliilima na kuitunza wala hapakuwa na magugu au miiba ya kuiharibu ardhi. Adamu na Hawa waliweza kufurahia vitu vyema ambavyo muumba mwenye upendo aliwapatia. Mungu aliamua kupima upendo wao kwake Mwanzo 2:15-17;3
MTI WA KUJUA MEMA NA MABAYA MWANZO 2:15-17
Katikati ya bustani ya Edeni Mungu alikuwa amepanda aina mbili za miti maalum “mti wa uzima” na “mti wa kujua mema na mabaya” Adamu na Hawa waliruhusiwa kula matunda ya miti mingine yote isipokuwa matunda ya mti huu wa pili. Mungu alisema, “Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapo kula matunda ya mti huo utakufa hakika. Walikuwa hawaruhusiwi hata kuugusa” (3:3)
Amri hii hakika ilikuwa rahisi ambayo Mungu aliwaonya kwamba ikiwa hawataizingatia watakufa hakika. Kutokutii sheria ya Mungu ni dhambi na “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23)
KUTOKUWA WATIIFU KATIKA EDENI MWANZO 3:1-6
Kwa muda mambo yaliendelea kuwa mazuri, lakini katika bustani hii ya Edeni kulikuwa na mnyama mwelevu aliyeitwa “nyoka” ambaye Mungu alimpa nguvu za kusema Mwanzo 3:15 hueleza jinsi nyoka aivyomwambia uongo na mwanamke alimwamini nyoka badala ya kumwamini Mungu. Nyoka kama walivyo wanyama wengine hakuwa na ufahamu wa kupambanua mazuri na mabaya kwani Mungu hakumpa akili kama alivyompa mwanadamu hata hivyo aliweza kusikia maagizo ya Mungu kwa Adamu na Hawa, lakini akidhani kwamba ikiwa watakula matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, bila shaka wangekuwa na ufahamu kama malaika. Hivyo alimwambia Hawa kuwa hakika “hamtakufa”.
Mara baada ya mawazo haya kumwingia Hawa akilini alianza kuushangaa mti ule. Aligundua kuwa ulikuwa ni “mti mzuri kwa chakula” na “unatamanika kwa maarifa”; na kadri alivyoyangalia matunda yake ndivyo alivyozidi kutamani mti ule. Na kuwa ungemwezesha kuwa mwerevu kama malaika, kama nyoka alivyokuwa amemshauri……. ghafla, Hawa alinyoosha mkono wake na kuchuma tunda na kula. Hatimaye alimpatia Adamu “ambaye pia alikula”.
Hawa alidanganywa na nyoka na hakutii amri ya Mungu. Adamu alitenda dhambi kwa kuchagua kumpendeza mkewe kuliko kumpendeza Mungu.
DHAMBI HULETA AIBU NA WOGA MWANZO 3:7-13
Mara baada ya Adamu na Eva kula tunda walijitambua kuwa wametenda dhambi. Ghafla walijukuta wanaona aibu na kuogopa. Kwa hiyo walishona majani ya mtini kuwa nguo za kujifunika. Walijificha katika bustani wakijua kuwa Mungu angekasirika. Na hivi ndivyo hutokea kwetu pia mara tutendapo dhambi. Mara tu tunapogundua kwamba tumekosea njia ya Mungu tunaona aibu na kujiona kuwa tu wenye hatia kwa Mungu.Wakati Mungu alipomwita Adamu, mkosaji Adamu alimlaumu Hawa na Hawa alipulizwa na Mungu naye alimlaumu nyoka. Lakini walikuwa wao wenyewe ndiyo waloijua sheria ya Mungu na ni wao walikuwa hawakuitii.
ADHABU YA MUNGU MWANZO 3:14 – 20
Kwa Nyoka: Kwa kuwa nyoka alisema uongo na kumdanganya Hawa, Mungu alimlaani. Atakwenda kwa tumbo na kula mavumbi katika siku zote za maisha yake.
Kwa Adamu: Mungu alimwambia Adamu kwamba badala ya kuishi katika bustani nzuri ambamo kila kitu kilikuwepo kwa kusudi la Mungu, watafukuzwa katika bustani hiyo. Tangu wakati huo na kuendelea ikamlazimu kufanya kazi kuwa ngumu ili kumwezesha kupata chakula chake na Hawa. Nchi sasa itaotesha miiba na magugu na kuifanya kazi kuwa ngumu zaidi. Mwishowe Adamu atafariki na kurudi tena katika mavumbi ya ardhi ambayo katika hayo aliumbwa kwa maana Mungu alisema, “kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi” (mstari 19). Mtu kwa hiyo akawa kiumbe cha kufa kwa sababu ya dhambi kwa maana “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23) kwa kuwa sisi sote tunatokana na ukoo wa Adamu tunashiriki pia katika namna moja ya asili na hivyo tunakufa.
Kwa Hawa: Hawa aliambiwa atakuwa na uchungu mno na kutawaliwa ma mmewe.
MUNGU ANAWAPATIA MAVAZI:14-20
Adamu na Hawa walikuwa wamejifunika majani ya mtini kujaribu kuficha aibu yao, lakini jambo hili halikukubaliwa na Mungu. Badala yake aliwapatia wote vazi lililotengenezwa kwa ngozi ya mnyama. Mungu alikuwa na sababu nzuri sana kwa ajili ya hili maana ilimfundisha Adamu na Hawa kuhusu dhambi. Kwa kuwapatia ngozi ni sharti kuwa mnyama lazima achinjwe na damu yake kumwagika. Yote haya yanatuelekeza mbele kwenye kifo chake Bwana Yesu Kristo ambaye kwa ajili ya kifo chake yetu Mungu alitutengenezea njia yetu ili dhambi zetu ziweze kufutwa au kusamehewa. Wakati mtu anapobatizawa, Biblia inasema kuwa mtu huyu anakuwa “amemvaa Kristo” (Wagalatia 3:27), kama vile Adamu alipojifunika vazi alilopewa na Mungu.
KUFUKUZWA KUTOKA KATIKA BUSTANI: MWANZO 3.22-24
Baada ya Mungu kuwaambia Adamu na Hawa kuhusu adhabu watakayopata kutokana na dhambi yao, Aliwafukuza kutoka katika bustani ya Edeni. “Ili wasije wakala matunda ya mti wa uzima ambapo wataishi milele”, kwa hiyo Mungu aliwafukuza kutoka katika bustani na akawaweka makerubi upande wa mashariki ya Bustani wakiwa na upanga wa moto uliogeuka huku na huko kulinda njia ya uzima (mistari 22-24).
FUNDISHO KWETU
Nirahisi sana kujaribiwa kutenda mabaya. Kosa la kwanza la Hawa lilikuwa kusikiliza maneno ya nyoka. Ikiwa tunasikiliza ushauri wa wale wasioipeda Kweli,na sisi pia tutamkosea Mungu. Njia pekee ya kuhakikisha kuwa tunamtii Mungu ni kuyaweka maneno yake akili mwetu “moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi” (Zaburi 119:11).
Dhambi ililetwa duniani kutokana na kosa la mtu mmoja kukosa utii, na kwa kuwa sisi ni watoto wa Adamu, ni lazima na sisi tufe pia. Lakini Mungu hataki watu wote wafe milele, kwa huruma yake, Aliiweka njia ya kusamehewa dhambi zetu kupitia ubatizo katika Bwana Yesu Kristo.
Jifunze kupenda sheria za Mungu na kuziweka ndani ya moyo wako, ili uweze kukua hadi kubatizwa hatimaye kupata karama ya Mungu ya uzima wa milele (Warumi 6:23).
MAELEZO YA ZIADA
Katika Mwanzo 3:15 Mungu anasema juu ya uadui, ambo daima utakuwepo kati ya uzao wa nyoka na uzao wa Mwanamke. Uzao wa nyoka ni wale wote ambo hawajui njia za Mungu na hawapendi Kweli. Uzao wa mwanamke ni wale wote wanaosema Kweli (kama Hawa alivyofanya kwanza. Mwanzo 3:2-3).
Kuna mmoja tu ambaye ametii kwa ukamilifu kwa kuitii Kweli; naye huyo ni Bwana Yesu Kristo. Tunaambiwa kwamba uzao wa nyoka “utamponda kisigino” (Mwanzo 3.15). Hili lilitimiaa wakati maadui wa Kweli (wayahudi waovu na Warumi) walipomwua msalabani. Kwa ajili ya utiifu wake mkamilifu kwa Mungu hakubaki kaburini, lakini Mungu alimfufua baada ya siku tatu.
“Mashambulizi ya” nyoka kwa Yesu yalikuwa ni “majeraha” aliyopata ambayo yalipona. Hata hivyo “Uzao wa mwanamke” hata hivyo “ungeponda kichwa” cha uzao wa nyoka (Mwa 3:15). Haya yangekuwa mashambulizi ya kifo kwa sababu Bwana Yesu Kristo alifufuka kutoka kaburini ili asife tena, dhambi na kifo vimepoteza nguvu. Ameviharibu na kufungua njia ya uzima wa milele kwa wale wote wanoipenda Kweli na kuweka tumaini katika yeye.
MASWALI
Majibu Mafupi
Ni amri ipi moja ambayo Mungu aliwapa Adamu na Hawa?
Ni nani alimsahwishi Hawa kuvunja amri hii?
Dhambi ni nini?
Mungu alisema jambo gani lingetokea ikiwa Adamu na Hawa watatenda dhambi?
Ni jambo gani linalowatokea watu wote kwa sababu ya dhambi ya Adamu na Eva?
Ni aina gani ya vazi ambalo Mungu aliwapatia Adamu na Eva?
Mungu alifanya nini baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi?
Majibu ya Kina.
1. Ni kwa jinsi gani Adamu na Eva hawakuitii amri ya Mungu katika bustani ya Edeni?
2. Ni kwa jinsi Mungu alivyowaadhibu Adamu na Eva Kutokana na kosa lao?
3. (a) Ni vazi gani kwa ajili ya dhambi ambalo Mungu aliwapatia Adamu na Eva?
(b) Je, tendo hili linamwonyesha nani?
Majibu ya Ziada
4. Eleza nini kilitokea baada ya Adamu na Hawa kula tunda la mti?
5. “Mshahara wa dhambi ni mauti,bali karama ya Mungu ni uzima wa milele”. Hii ina maana gani?
6. Eleza maana ya yafuatayo:
(a) Uzao wa nyoka
(b) Uzao wa mwanamke
(c) Huo utaponda kisigino chake; na
(d) wewe utakiponda kichwa chake
0 notes
Text
MUUZA CHIPS (42)
Jina: MUUZA CHIPS Mwandishi: MoonBoy SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI ILIPOISHIA... Ikabidi walipite mpaka kwenye kituo cha mbele, mana kuna wengine walipanda lakini wanashukia njiani kama vile walisogezwa tu,.. Sasa pale pale chidi akapanda kwenye basi huk
Jina: MUUZA CHIPSMwandishi: MoonBoy SEHEMU YA AROBAINI NA MBILIILIPOISHIA… Ikabidi walipite mpaka kwenye kituo cha mbele, mana kuna wengine walipanda lakini wanashukia njiani kama vile walisogezwa tu,.. Sasa pale pale chidi akapanda kwenye basi huku akipumua kwa nguvu zote, kana kwamba kafanikiwa alichokifuata japo abiria ni wengi sana, lakini hakukata tamaa KAMA UNATUMIA APP WAKATI UNAFUNGUA…
View On WordPress
0 notes
Photo
Kingine alichotisha #KingKiba Katika #fungamwakanakingkiba Ni kumpandisha Jukwaani Upcoming Artist @kayumbaasosie Na Baadae akapanda @officialalikiba na Kuimba nae, Kitu ambacho ni aghalabu kutokea kwa Msanii wa Kimataifa aliesainiwa na Sony Music kufanya kitu kama hicho kwa Up coming artist asiekua ame sainiwa na Record label kubwa yeyote, asiekua na Wazfa wa kumlipa Msanii mkubwa . Kumaanisha Kuanzia Ucku wa Jana #Kayumba Ni Msanii wa kuangaliwa sana, kama Kiba amefanya vile basi Taarifa zimetufikia watanzania Kuwa Kayumba sio Msanii wa kumchukulia Poa Poa tena, Ana kitu kikubwa na atakuja kuwa mkubwaaaaaaa https://www.instagram.com/p/BsAePvdhhVG/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=1qpb1xnbsp280
0 notes
Photo
#arusha #Tanzania 2018 . @mahealbarwani a first Oman who entered Africa Continent by his motorbike...he started his journey 22/07/2017 it's has been more than a year since he started his journey from Oman entered the Emirates,Saudi Arabia he took ferry to cross Sudan,Ethiopia,Kenya,Uganda,Rwanda, Burundi and enter Tanzania.He visited Tanzania regions up to Dar Es Salaam,took the ferry to Zanzibar Island with his motorbike,then again took another ferry to Pemba,then to Tanga and road transfer with his motorbike to Arusha and Moshi.He still continuing with his journey to other remaining regions and then heads to South Africa.. . Please follow him on his Instagram and support him more. #maheralbarwani . @maheralbarwani muoman wa kwanza alieingia bara la Africa peke yake kwa kutumia pikipiki tu ... alianza safari yake 22/07/2017 ni zaidi ya mwaka mmoja toka alipoanza safari yake kutoka Oman aliingia Emirates, Saudia kapanda meli kuingia Sudan, Ethiopia, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi kisha akaingia Tanzania alizunguka mikoa ya Tanzania mpaka kufika Dar es salaam alipanda meli kuelekea Zanzibar na usafiri wake wa pikipiki, alafu akapanda meli na kuelekea Pemba na usafiri wake wa pikipiki baada ya Pemba alipanda meli na usafiri wake Tanga alafu Moshi kuja Arusha. bado anaendelea na safari yake kumalizia baadhi ya mikoa mengine ilobakia na kuelekea South Africa.. . Please mfollow kwenye instagram yake tumpe support zaidi. #maheralbarwani (at Arusha, Tanzania) https://www.instagram.com/p/BncDENdDmFv/?utm_source=ig_tumblr_share&igshid=xrdy5wasub9l
0 notes
Photo
Parables Mwanzo World kuwa empty. Spirit flying over. Then word ikafika.Akatenganisha mbingu na ardhi hatuezi kana, creativity ilikua testimony ya kwanza kufika hapa.six days God by word of mouth creation inakam to life kaa mmea.then on the sixth day akapanda mbegu.
0 notes
Photo
How was your Sunday?#Jumapili yako ilikuwaje? 1 Then Jesus entered and passed through Jericho. 2 Now behold, there was a man named Zacchaeus who was a chief tax collector, and he was rich. 3 And he sought to see who Jesus was, but could not because of the crowd, for he was of short stature. 4 So he ran ahead and climbed up into a sycamore tree to see Him, for He was going to pass that way. 5 And when Jesus came to the place, He looked up and saw him, and said to him, “Zacchaeus, make haste and come down, for today I must stay at your house.” 6 So he made haste and came down, and received Him joyfully. 7 But when they saw it, they all complained, saying, “He has gone to be a guest with a man who is a sinner.” 8 Then Zacchaeus stood and said to the Lord, “Look, Lord, I give half of my goods to the poor; and if I have taken anything from anyone by false accusation, I restore fourfold.” 9 And Jesus said to him, “Today salvation has come to this house, because he also is a son of Abraham; 10 for the Son of Man has come to seek and to save that which was lost.”#Luke 19:1-10 ��Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa akipita katika njia za mji huo. Palikuwa na mtu mmoja huko mjini aitwaye Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watozaushuru, na pia mtu tajiri. Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu. Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo. Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.” Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha. Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunungunika wakisema, “Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi.” Lakini Zakayo akasimama, akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyanganya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.” Yesu akamwambia, “Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu. Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”” Luka 19:1-10#wordofthenight🌓#weekend#sundayblessings#church#faith#kanisani#beblessed#Lifestyleblogger#RachelSiwa🙏🏽❤
#church#luke#wordofthenight🌓#jumapili#rachelsiwa🙏#beblessed#kanisani#sundayblessings#lifestyleblogger#weekend#faith
0 notes
Photo
HEART EYES 193 Dorice nae ni mrembo japo kazidiwa kiasi na Maisarah ni msichana msomi na mwenye kazi nzuri katika ofisi ya raisi, anakaa pembeni ya Feroz, anaweka mkono wake kwenye zipu ya suruali ya Feroz I miss you honey, sikia you were once mine but now I know your not ila hauko sawa, I'm not comitted Feroz nashindwa kupenda sababu nilikupenda sana ukaniacha kwenye mataa. Nimeshasahau though sijausahau utamu wa mapenzi yako so let me give you some good time okey? I don't need you to be commited to me neither do i, wala sitaki unilipe it's a free service Dorice anamaliza kisha anaingiza mkono wake ndani ya t-shirt ya Feroz, anamgusa tumbo kwa mikono yake laini bila kujali wako sehemu ya wazi Dor No Feroz don't say anything sijaomba kuwa mpenzi wako so just think of me as a bitch Dorice your not Umeshawahi kununua mwanamke? No Buy me today then hautakua na regrets cause nitakua kama malaya wanaojiuza No Dorice No Feroz leo mimi nitakua na final say Dorice ananyanyuka, anaenda reception na kukilipia chumba anarudi pale It's done utanikuta chumba namba 311 Anaondoka bila kusubiri jibu la Feroz, Feroz anamtazama anavyomtingishia makusudi anainuka anamfata nyuma, Dorice anapofungua mlango tuu kabla hajafunga Feroz anashika kitasa hakua amejua kama yuko nyuma yake maana Feroz alimsubiri apande lift na yeye ndo akapanda. Anamshika kiuno, anafunga mlango na kumpa alichokililia lakini mawazo yake yakiwa kwa Maisarah, anashinda na Dorice hadi saa 1 jioni anarudi nyumbani, anamueleza Leandra kilichomkuta na Maisarah Leandra anamwambia asiwaze. Maisarah kuanzia amemuona Feroz anakosa raha, anatamani kumpigia simu anaogopa vitisho vya Brown kwa Feroz, anamtafuta mama yake hewani hampati anaamua kwenda Sinza siku inayofuatia Mama yako kasafiri mbona hamjaagana? Mpangaji anamwambia Maisarah anaeshikwa na mshangao mkubwa Mchumba wako alikuja kumsafirisha juzi, na leo wapangaji wamekuja kuangalia wanahamia huku kwenu Maisarah anahisi kuchanganyikiwa, ikiwa ni wiki moja tuu imebaki kabla ya harusi yake. Anajihisi mpweke sababu hana marafiki kama zamani, ni Brown na watu wake ndo wanashughulikia mambo yake, anaanza kuona jinsi maisha yake yatakavyokua ya upweke baada ya ndoa...
0 notes
Photo
Siku moja nilimnyandua dada mmoja vizuri mpaka tulivyofika stendi akanikumbatia na kunibusu kwa mahaba kisha akapanda daladala akaondoka, nilibaki nacheka sana Kuna jamaa alikuwa amekaa nyuma yangu akaniuliza "Kaka mbona unacheka?" nikamjibu "Huyu dada ndio anakaa hapa mimi nilikuja kumtembelea tu, sasa nashangaa yeye ndio kapanda daladala na kuondoa" #ChekanaZephiline (at Cheka na Zephiline) https://www.instagram.com/p/CMLA8loJ4-h/?igshid=zg3m06uuuich
0 notes
Text
akapanda replied to your post: im 4 streets away from the flooding im v scared...
My neighbourhood had to evacuate this morning at 1am LOLOL fml
ARE YOU SERIOUS? do you have a place to stay oh my god are you safe
2 notes
·
View notes
Note
Omg LOL nvm scratch that Mind if i stand next to you cause someone farted over there
hahaha i know im cool to stand beside you;)
0 notes
Photo
Tumblr Crushes:
fuckyeahmadasiancuties
damnanniee
fkyeahitspaul
nut-e-l-l-a
akapanda
rinadesu
0livia-dawood
sithaohsodope
jayyfuckenlegit
#fuckyeahmadasiancuties#damnanniee#fkyeahitspaul#nut-e-l-l-a#akapanda#rinadesu#0livia-dawood#sithaohsodope#jayyfuckenlegit
0 notes